Mgombea wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha National Reconstruction Allience (NRA) Hassa Almasi na mgombea mwenza Hamis Hassa Majukumu wamefika Ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Wawili hao wamefika katika ofisi ya INEC mtaa wa Njedengwa saa 7:55 mchana na kupokelewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC Ramadhani Kailima.Katika msafara huo waliongozana na watu wengine waliokuwa kwenye magari madogo matatu yaliyofungwa bendera za chama
NRA haikuwa na msafara mkubwa ukilinganisha na msafara wa CCM,Mgombea huyo ametumia dakika 22 kisha akatoka na akazungumza na vyombo vya habari na Almasi amesema wanamini wao ni washindi katika uchaguzi kuwa Mungu awapiganie ili washike Dola.
.jpg)
0 Comments