Header Ads Widget

MWALIMU MKUU AUAWA KWA KITU CHA NCHA KALI SHINYANGA


Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Busalala,Kata ya Mwenadakulima,Kahama mkoani Shinyanga Fatuma Khamis ameuawa kwa kuchomwa shingoni na kitu cha ncha kali na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Agosti 9,2025.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.Amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa Fatuma alikuwa na ugomvi wa kifamilia baina yake na mumewe na kwamba mpaka sas wanamshikili mume wa marehemu kwa uchunguzi zaidi.

Amesema,aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali uapnde wa kaulia wa shingo yake na watu wasiofahamika.Upelelezi wa awali palikuwa na ugomvi wa kifamilia,hivyo sasa hivi tunaendelea kupeleleza ili kuweza kujua nini kiini chga tukio hili,na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya manispaa ya Kahama.

Amesema vitendo vya uakatili hususani wa kimwili,vimepungua mkoani humo na kwamba Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea kutoa elimu kwa wanandoa kuepuka vitendo hivyo kwani ni kinyume cha sheria

 

Post a Comment

0 Comments