Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) wameanza kujiongea ukumbini tayari kwa kutekeleza shughuli yao ya kuwachagua watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Rais wa Zanzibar Oktoba 29,2025.
Jumla ya majina matano yanatarajiwa kuwasilishwa mbele ya wajumbe hao,baada ya kupitishwa na kufanyiwa mchujo na Kamati ya Uongozi,kisha Baraza Kuu la chama hicho na kujiridhisha wamekidhi vigezo,hivyo ni kazi ya wajumbe kumchagua wanayefaa.
Kati yao,watania wawili wanawania nafasi ya Rais,ambao ni Mkunyutila Siwale na Samandito GFombo huku Rose Kohoji ambaye pia alitia nia, jina lake limeondolewa na Baraza Kuu la Chama hicho kwa kosa la kuunga mkono walioleta vuruguzilizofanyika Agosti 6,2025 katika kikao cha Baraza Kuu la Chama hicho.
Kwa upande wa Zanzibar,makada watatu waliotia nia wote wamepenya ambao ni Habibu Mohamed,Masoud Hamad na Mohamed Khatib,wote watafikishwa mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu ili wamchague mmoja wao atakaye peperusha bendera ya chama hicho upande wa Zanzibar.
.jpg)
0 Comments