Header Ads Widget

UCHAGUZI WAANZA KUPAMBA MOTO SAMIA ACHUKUA FOMU RASMI INEC


Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ccm Samia Suluhu Hassan na Mgombea mwenza Dkt Emmanuel Nchimbi rasmi wachukua fomu ya Urais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (inec) leo Agosti 9,2025.

Maelfu ya wanachama na wananchi kwa ujumla ambao wanamuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan wafurika katika shamra shamra za uchukuaji wa fomu Jijini Dodoma leo katika ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi.

Katika hatua hii inaonesha wazi kuwa shamra shamra za mbio za uchaguzi mkuu Oktoba 29,2025 imekwisha gonga hodi sasa ni mambo moto katika mbio hizo.

Samia amechukua hatua hiyo ya kuchukua fomu ili kutimiza kanuni moja wapo katika kueleka uchaguzi mkuu wa Tanzania Oktoba 29.

Akizungumza leo Agosti 9, 2025 baada ya kuchukua Fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha #CCM Rais Samia amesema, "Serikali inayowekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) inauzoefu Mkubwa, tuna uzoefu mkubwa katika kutekeleza, sisi sio Wanafunzi hata kidogo, wengine wote inabidi waanze kujifunza kwanza."

Post a Comment

0 Comments