Header Ads Widget

Dkt. Samia Suluhu Hassan Aendelea Kuinadi Ilani ya CCM Kigoma, Akiahidi Kuendeleza Miundombinu na Biashara


 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 14, 2025, anafanya mkutano wa kampeni Kigoma Mjini, ukiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Wilaya za Kasulu, Uvinza na Buhigwe, kwa lengo la kuinadi Ilani ya CCM katika mikoa ya Kanda ya Magharibi.


Katika mkutano huo, Dkt. Samia atawanadi pia wagombea ubunge wa majimbo yote ya Mkoa wa Kigoma, akisisitiza mshikamano wa chama na dhamira ya kuendelea kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi mkoani humo.


Awali katika mikutano yake katika mkoa huo, Dkt. Samia aliwahakikishia wananchi kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha biashara na lango kuu la kiuchumi kwa nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Aidha, aliweka mkazo katika kuendeleza miundombinu, kuboresha upatikanaji wa nishati, na kuvutia wawekezaji, huku akibainisha mradi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma kama chachu ya kukuza biashara, ajira, na ukuaji wa sekta za Kilimo, Uvuvi, na Viwanda.


Dkt. Samia amesisitiza kuwa maendeleo ya Kigoma ni sehemu ya dhamira ya CCM ya kuimarisha uchumi wa wananchi na kuleta uwekezaji endelevu katika mikoa ya Magharibi.

Post a Comment

0 Comments