Header Ads Widget

Manara: ‘Niachieni Mimi, Nitapigania Kariakoo Mpya’




Mgombea udiwani kata ya kariuakoo kupitia CCM,Haji Manara ameahidi kutatua kero ya maji taka,kukatika kwa umeme inayolikabili eneo maarufu la biashara la kariakoo,wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.

Sambamba na hilo ameahidi kulinda heshima ya wafanyabiashara wa kariakoo ambapo amesema wanalipa kodi kubwa hapa nchini,hivyo mazingira bora ya kufanyia biashara yanastahili kuboreshwa.

Manara ameyasema hayo leo  katika uzinduzi wa kampeni za udiawani kata ya kariakoo zilizohudhuliwa na wagombea wa chama hicho wilaa ya Ilala akiwemo mgombea ubunge jimbo la Ilala,Mussa Zungu.

Amesema kariakoo ni kongwe kitovu cha biashara na yenye historia,Tunasema inalipa kodi sana hivyo shida kama umeme,maji na taka na safi lazima tutatue hapa kuna wafanyabiashara na wakaazi ni lazima tulinde masilai ya wote amesema

Amesema haiwezekani umeme kukatika mara kwa mara pia maiji kuwa keroi kwa eneo linalolipwa kodi kwa wingi.kuhusu wafanyabiashara ndogondogo amesema atasiamamia na serikali katika kuwawekea mazingira bora
 

Post a Comment

0 Comments