Akizungumza leo tarehe 15 Septemba 2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Gombani ya Kale, Wilaya ya Chake Chake, Kusini Pemba, Dkt. Mwinyi alisema kukamilika kwa uwanja huo wa kisasa kutaifanya Pemba kuwa kitovu cha utalii na biashara, kwani ndege kubwa kutoka nje ya nchi zitaweza kutua moja kwa moja kisiwani humo.
Akiwa mbele ya maelfu ya wananchi, alitaja hatua muhimu zilizochukuliwa na Serikali yake katika kuimarisha maendeleo ya Zanzibar, ikiwemo:
- Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kisasa Pemba
- Ugawaji wa hati miliki kwa mashamba ya karafuu
- Kukamilika kwa barabara ya Chake Chake – koani
- Mradi wa nyumba 10,000 za gharama nafuu Unguja na Pemba
- Kuimarisha uwekezaji na viwanda kwa ajili ya kuongeza ajira kwa vijana
Dkt. Mwinyi aliwaomba wananchi wa Pemba kumpa ridhaa nyingine ya kuendelea kuongoza Zanzibar, sambamba na kumpa kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa CCM katika nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani.
“CCM itaendelea kuwa chama cha mshikamano, amani na maendeleo. Tunataka kampeni zetu ziwe za hoja, si za kuchochea mfarakano,” alisisitiza Rais Mwinyi.

0 Comments